Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WIZARA YA MALIASILI NA UTALII Simu Na: +255 026 2321566 Mtaa wa Kilimani, Nukushi: +255 026 2321514 Barabara ya Askari. Barua pepe: Qs@mnn.go.tz S.L. 1351. 40472-DODOMA Wizara ya Maliasili na Utalii inautaatifu umma kuwa, taarifa iliyotolewa tarehe 09 Mei, 2018 na Taasisi ya Oakland iliyopo nchini Marekani ikiwa na kichwa cha habari ?Losing the Serengeti: the Maasai land that was to rm forever? na kunukuliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza-BBC Swahili kwa kichwa cha habari "Tanzania yadalwa kukandamiza bald za Wamaasal wanaoishi Loliondo' ni potofu. Taarifa hiyo imeituhumu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa imefanya; uchomaji wa makazi kwa jamii ya wamasai, kuondoa mifugo yao kutoka kwenye maeneo ya malisho na maji, kuwatesa wananchi na kuwazuia kutoa maoni yao, taarifa ambazo si za kweli. Ukweli ni kuwa, kutokana na umuhimu wa eneo hilo kwa uhifadhi, uwepo wa vyanzo vya maji, eneo Ia mzunguko wa uhamaji wa wanyamapori na maisha ya watu, Serikali kupitia Oflsi ya Waziri Mkuu ilichukua hatua stahiki za kutatua mgogoro huo ikihusisha wadau wote muhimu yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, wawekezaji pamoja na wananchi. Kazi hiyo inaendelea na Serikali itatoa taarifa rasmi kuhusu suala hili. Wizara ya Maliasili na Utalii inawataka watanzania na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo potofu yenye lengo la kuipaka matope Serikali na kuleta uchonganishi baina yake, wananchi na wawekezaji kwa lengo la kuleta uvunjifu wa amani. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau wenye nia njema kwa uhifadhi na maendeleo ya wananchi katika kusimamia na kuendeleza rasilimali zilizopo katika eneo la Loliondo na maeneo mengine nchini kwa maslahi mapana ya Taifa. 144 Mg Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb) Waziri wa Maliasili na 10 Mei, 2018